BYH programu
Ni programu inayotoa ushauri wa mlo lishe kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi(HIV).
Mhusika anaweza kuingiza aina ya chakula anachokula ndani ya siku na kupata ushauri juu ya mpangilio wa mlo wa chakula.
BetterYourHealth ni mradi uliozinduliwa katika manispaa ya kinondoni chini ya mdhamini wa Tanzania Data lab (dlabs)
BetterYourHealth kwa kushirikiana na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni,Afisa lishe Bi.Janeth Mnzava waliweza kufanikiwa kuzindua vituo ishirini(20) katika Manispaa ya wilaya ya Kinondoni baadhi ya maeneo kama Bunju, Magomeni, Kawe, Kigogo, Madale n.k